12 Septemba 2015 - 21:58
 Waziri wa mambo ya ndani Uganda afariki Dunia

Jenerali Aronda Nyakairima waziri wa mambo ya ndani nchini Uganda amefariki dunia huko Dubai wakati akiwa safarini akitokea Korea Kusini ambapo alikuweko kwa shughuli rasmi za kiserikali.

Shirika la habari la ABNA linaripoti kuwa: Jenerali Aronda Nyakairima waziri wa mambo ya ndani nchini Uganda amefariki dunia huko Dubai wakati akiwa safarini akitokea Korea Kusini ambapo alikuweko kwa shughuli rasmi za kiserikali. Nyakairima aliwahi kuwa mkuu wa majeshi nchini Uganda kwa muda wa miaka kumi kabla ya kuteuliwa kuwa waziri wa mambo ya ndani.Taarifa ya Waziri Mkuu wa Uganda Dr. Rukahama Rugunda imesema serikali imeunda kikosi kazi kinachoongozwa na Waziri wa Ulinzi Dr.Crispus Kiyonga kuratibu masuala yote kuhusiana na kifo hicho cha ghafla ambacho sababu yake haijulikani.Timu ya madaktari bingwa wa elimu ya magonjwa pia inapelekwa Dubai Umoja wa Falme za Kiarabu kusaidia uchunguzi wa kile kilichopelekea kifo chake na kuurudisha mwili nyumbani.Jenerali huyo anatajwa kuwa mmoja kati ya watu waaminifu na watiifu kwa utawala wa Rais Yoweri Museveni.Kile ambacho kitakuwa cha kumbukumbu kwa kila Mganda ni juhudi alizofanya Nyakairima kuhakikisha kuwa mpango wa kutoa vitambulisho vya kitaifa kwa mara ya kwanza unafaulu.Kifo cha Nyakairima kimetokea wakati akiandaa mikakati ya usalama kuhusiana na uchaguzi mkuu ujao.

Mwisho wa habari/ 291